KIPRE TCHETCHE YUPO FITI SASA KUIVAA SIMBA SC JUMAPILI


MSHAMBULIAJI hatari wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Kipre Tchetche, yupo fiti asilimia 100 kuivaa Simba  kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kesho kutwa Jumapili.

Mchezo huo ni muhimu kwa Azam FC inayodhaminiwa na Benki ya NMB katika kuendeleza mbio za kuwania ubingwa wa ligi hiyo walioupoteza msimu uliopita baada ya kuchukuliwa na Yanga.

Tchetche aliyeanza kufanya mazoezi na timu tokea timu hiyo ikijiandaa na mechi dhidi ya Majimaji, alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya enka aliyopata kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar uliofanyika Uwanja wa Manungu, Morogoro ambao Azam FC ilishinda bao 1-0 lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na nahodha John Bocco ‘Adebayor’.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Stewart Hall, ameuthibitishia mtandao wa klabu www.azamfc.co.tz leo kuwa Tchetche yupo fiti kwa ajili ya mchezo huo baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yakimkabili.
Katika hatua nyingine kiungo Frank Domayo, aliyepata maumivu ya enka wakati wa mchezo wa Mwadui, yeye atakuwa fiti baada ya wiki mbili zijazo na sasa anaendelea na matibabu chini ya jopo la madaktari wa Azam FC.

Kuhusu uwepo wa wachezaji wengine kama vile Pascal Wawa, Allan Wanga, Wazir Salum, Racine Diouf  itajulikana mara baada ya mazoezi ya mwisho ya Azam FC kesho kabla ya kuwavaa Wekundu hao wa Msimbazi.

Kiungo Himid Mao 'Ninja' yeye ataendelea kukosekana kutokana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata kwenye mchezo namba 170 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Azam FC iliyobakisha michezo mitano ya ligi, mpaka sasa inashika nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa imejikusanyia pointi 58, Simba yenyewe imejizolea pointi 57 katika nafasi ya tatu huku Yanga ikiwa kileleni baada ya kufikisha pointi 62.

Jedwali la msimamo wa ligi ya EPL kufikia 19 Aprili, 2016.


Mwandae Mchungulike



 Jedwali la msimamo wa ligi ya EPL kufikia 19 Aprili, 2016.

Nambari Klabu Mechi Mabao Alama
1 Leicester 34 26 73
2 Tottenham 34 39 68
3 Man City 33 28 60
4 Arsenal 33 22 60
5 Man Utd 33 10 56
6 West Ham 33 12 53
7 Southampton 34 10 51
8 Liverpool 32 9 51
9 Stoke 34 -10 47
10 Chelsea 33 4 44
11 Everton 33 9 41
12 Watford 33 -5 41
13 Bournemouth 34 -16 41
14 West Brom 33 -9 40
15 Swansea 34 -11 40
16 Crystal Palace 34 -7 39
17 Norwich 34 -25 31
18 Sunderland 33 -18 30
19 Newcastle 33 -26 28
20 Aston Villa 34 -42 16
 msimamo mpya wa ligi kuu baada ya mechi za jana 3/4/2016

msimamo mpya wa ligi kuu baada ya mechi za jana 3/4/2016

   

Michezo ya viporo ya Ligi Kuu soka Tanzania bara imepigwa leo kwa vilabu vya Azam FCna Yanga kucheza michezo yao ambayo awali ilikuwa imehairishwa kutokana na kuingiliana na michezo yao ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, lakini na michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa upande wa Yanga
                           Matokeo ya mechi za jana
8

                 
            Ufuatao ndio   Msimamo wa Ligi Kuu kwa 10 za juu
1

Kategori

Kategori