Usiku wa kuamkia leo kumechezwa michezo ya kirafiki ya kimataifa ikiwa ni michezo ya kujiandaa na michuano ya kombe la ulaya. Mabingwa
wa kombe la dunia mwaka 2010 Hispania walitosha nguvu na itali kwa
kufunga bao 1-1,Uturuki wakapata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Swedeni. Malta
wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani wameambulia sare ya 0-0 na
Moldova, Norway na Estonia nao wakashindwa kutambiana baada ya kwenda
sare ya bila bila. Matokeo mengine Ugiriki 2-1 Montenegro 1 Denmark 2 -1Iceland 1 Ukraine 1-0 Cyprus 0 Jamuhuri ya Czech 0-1 Scotland wales 1-1 Ireland ya kaskazini
Michezo ya kusaka tiketi ya kushiki michuano ya kombe la mataifa ya afrika mwaka 2017 itayofanyika Gabon itaendelea tena leo
Katika kundi A timu ya taifa ya Djibout itakua nyumbani katika uwanja wake wa Djibouty kukipiga na liberia.
Ghana maarufu kama the Black Stars walioko kundi H watakua wenyeji wa timu ya Mozambique wanaofahamika kama Mambas.
Comoros watashuka dimbani kuwakabili Botswana huku Madagascar akipimana ubavu na timu ya taifa ya Jamuhuri ya Africa ya kati.
Mbwana Samatta akivaa kitambaa cha unahodha kwa mara ya kwanza,
amekiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kupata
ushindi wa goli 1-0 ugenini dhidi ya Chad kwenye mchezo wa Group G
kuwania nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika
inayotarajiwa kufanyika mwaka 2017 nchini Gabon.
Mbwana Samatta amefunga goli hil kipindi cha kwanza akimalizia kazi
nzuri iliyofanywa na Farid Musa goli ambalo limedumu hadi dakika 90 za
mchezo huo.
Stars imefikisha pointi 4 baada ya kucheza michezo 3, matokeo hayo
yanaifanya Stars ifikishe idadi sawa ya pointi na Nigeria ‘The Super
Eagles’ lakini Stars ipo mbele ya Nigeria kwa mchezo mmoja. Nigeria
itakutana na Misri kwenye mchezo wa kundi ilo siku ya Ijumaa.
Stars itacheza mchezo wake wa marudiano dhidi ya Chad siku ya Jumatatu
March 28 mwaka huu kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Msimamo wa Group G unaongowa na Misri yenye pointi 6 ikifatiwa na
Nigeria na Tanzania zenye pointi 4 lakini Nigeria ikishika nafasi ya
pili kwa tofauti ya magoli wakati Chad ikiwa ya mwisho bila pointi.
Tanzania na Chad zimecheza mechi 3 mechu moja mbelea ya Misri na
Nigeria.
Matokeo ya mechi nyingine za kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika
kwa mechi ambazo tayari zimemalizika yapo kama ifuatavyo:
Aliyekuwa Nahodha
na kisha kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani iliyotwaa kombe la dunia
Franz Beckenbauer ametajwa katika orodha ya watuhumiwa 6 wanaoshukiwa
kutoa hongo kununua kombe la dunia la mwaka wa 2006 huko Ujerumani.
Kamati ya maadili ya FIFA imetoa orodha wa watu 6 waliongoza kampeini hiyo ya kutwaa uwenyeji wa kombe la dunia.
Shirikisho
la soka la Ujerumani lilipasua mbarika lilipofichua ripoti ya upelelezi
ambayo ilimpelekea Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani
kukiri kuwa alifanya makosa wakati wa kuwania zabuni ya wenyeji wa
kombe hilo la dunia.
Mnamo mwezi Oktoba mwaka uliopita,
Beckenbauer, 70, aliomba msamaha kwa hatua na kauli alizotoa wakati wa
kuwania uwenyeji wa mashindano hayo.
Ujerumani wakati huo iliishinda Afrika Kusini kwa kura moja pekee. Mnamo mwezi Oktoba mwaka uliopita, Beckenbauer, 70, aliomba msamaha kwa
hatua na kauli alizotoa wakati wa kuwania uwenyeji wa mashindano hayo.
Ujerumani ilipata kura 12 dhidi ya 11 za Afrika Kusini katika uchaguzi uliofanyika mwaka wa 2000. Orodha kamili
Franz Beckenbauer
Wolfgang Niersbach
Helmut Sandrock
Theo Zwanziger
Horst Schmidt
Stefan Hans
Beckenbauer aliiongoza kikosi cha taifa cha West Germany wakati huo kutwaa kombe la dunia la mwaka wa 1974.
Jarida la upekuzi la Ujerumani, Der Spiegel mwaka
uliopita liliripoti kuwa waandalizi wa kombe hilo walitenga Euro milioni
6.7 kununua uwenyeji wa mashindano hayo.
Beckenbauer, Zwanziger,
Schmidt na Hans awanachunguzwa kwa makosa ya kutoa hongo
ilikuwashawishi wajumbe waipigie Ujerumani kura pamoja na kutoa zabuni
kadhaa kwa wajumbe fulani.
Kwa upande wao Niersbach na Sandrock wanachunguzwa kwa kosa la kushindwa kuripoti ukiukwaji wa kanuni na maadili ya FIFA.
Beckenbauer aliiongoza kikosi cha taifa cha West Germany wakati huo kutwaa kombe la dunia la mwaka wa 1974.
Aidha aliifunza timu hiyo miaka 16 baadaye ilipoibuka mabingwa wa dunia nchini Italia.
Amewahi pia kuifunza timu za Marseille na Bayern Munich, ambako anaihumia kama rais.
Taifa Stars ya Tanzania imesafiri Chad kwa mechi ya kundi ya la G
Kenya, Tanzania na
Sudan Kusini zitakuwa uwanjani hapo kesho kutafuta tiketi ya safari ya
Gabon mwakani kwa mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika..
Kenya
iko ugenini dhidi ya Guinea Bissau kundi E, Tanzania imesafiri Chad kwa
mechi ya kundi ya la G huku Sudan Kusini ikiikaribisha ikiikaribisha
Benin mechi ya kundi C..
Mechi zingine zitakazochezwa kesho ni Sao
Tome wako nyumbani dhidi ya Libya kundi F na Zambia wanakaribisha Congo
kundi E, na kesho kutwa mechi ya kundi la B, Madagascar inapambana
nyumbani na Afrika ya Kati..
Harambee Stars ya Kenya itakuwa na
wachezaji wake wa kutegemewa wa ng'ambo wakiongozwa na kiungo mkabaji wa
Southampton Victor Wanyama, kipa Arnold Origi na Michael Olunga. Nahodha wa Kenya Victor Wanyama
Baada ya kucheza mechi mbili Kenya ni ya tatu na pointi moja tu, Congo ikiwa juu na pointi nne ikifuatiwa na Congo na Zambia..
Nahodha mpya wa Taifa Stars ya Tanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu ni tegemeo kubwa kwenye mechi yao na Chad.
Taifa
Stars ni ya tatu kundi G na pointi moja tu kwa mechi mbili walizocheza,
kwanza wakameza mabao matatu bila jibu kisha wakaenda sare na Super
Eagles ya Nigeria.
Misri inaongoza kundi hilo na pointi sita, Nigeria ya pili na nne.. Alex Iwobi wa Arsenal na Nigeria
Nigeria kwa sasa inaomba na kuamini kuwa nyota wa
Arsenal Alex Iwobi atapata afueni na kuiwakilisha taifa hilo Super
Eagles ya Nigeria itakapochuana na Firauni..
Sudan Kusini
inashikilia nafasi ya pili kundi C na pointi tatu huku Mali ikiwa juu na
nne, Benin ya tatu na Equatorial Guinea ya mwisho..
Mechi za marudiano zitachezwa wikendi hii kwa wanaocheza leo...
Mkurugenzi mkuu wa
maandalizi ya michuano ya tenisi huko Indian Wells Raymond Moore
amejiuzulu baada ya matamshi yake yaliozua utata kuhusu wanawake katika
mchezo huo.
Moore mwenye umri wa miaka 69,amesema kuwa mchezo wa
tenisi wa wanawake unategemea sana wanaume,maoni yalioelezewa kuwa ya
ubaguzi wa jinsia na muungano wa tenisi nchini Marekani USTA.
Mchezaji
nambari moja duniani kwa upande wa wanawake Serena Williams alisema
kuwa matamshi ya Moore yana kera na yasio ya ukweli.
Lakini mwenzake kwa upande wa wanaume Novak Djokovic alidai kuwa ziara yake inafaa kupigania wanaume wapewe fedha zaidi. Serana Williams
Moore alisema kuwa wachezaji wanawake wanafaa kuwapigia magoti wenzao wa kiume kama vile Roger Federer na Rafael Nadal.
Lakini mchezaji huyo wa zamani wa Afrika Kusini baadaye aliomba msamaha kwa matamshi yake.
Gwiji
wa mchezo huo Martina Navratilova alisema kwamba matamshi ya Moore
yanachukiza sana,akiongezea kuwa wachezaji wanawake huenda wakasusia
michuano ya Indian Wells iwapo Moore ataendelea kuwa mwandalizi. Novak Djokovic
Djokovic ambaye alishinda taji la BNP la Paribas
Open huko India Wells siku ya Jumapili aliyaelezea matamshi ya Moore
kama yasio sawa.
Lakini raia huyo wa Serbia mwenye umri wa miaka
28 alihoji kwamba wanaume wanafaa kupewa fedha zaidi kwa sababu watu
wengi huangalia mechi zao.
Golikipa wa kimataifa ya Jamuhuri ya Czech Petr Cech ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa nchi hiyo.
Cech
Mwenye umri wa miaka 33,alichaguliwa na makocha, wachezaji na viongozi
wa timu kutwaa tuzo ya nane ya uchezaji bora nchini mwake.
Golikipa
huyu amewazidi wachezaji wenzake wa timu ya taifa Mshambuliaji wa
Sparta Prague David Lafata, na kiungo wa Vladimir Darida anayeichezea
Hertha Berlin.
kipa huyu wa klabu ya Soka ya Arsenal ameichezea timu ya taifa michezo 118 tangu alipoanza soka la kimataifa mwaka 2002.
Timu ya taifa ya
Tanzania Taifa Stars itashuka dimbani hapo kesho, huko nchi Chad katika
mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2017.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 11 kwa saa za nyumbani Afrika Mashariki.
Taifa
Stars, imefanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo huo katika uwanja wa
Omnisports Idriss Mahamat Ouya ulipo katika jiji la D'jamena.
Kocha
anayekinoa kikosi hicho Charles Boniface Mkwasa amesema anashukuru
vijana wake hakuna majeruhi na wote wameweza kufanya mazoezi
aliyoyapangilia.
England iko mbioni kumzuia nyota wa Arsenal Alex Iwobi asijiunge na timu ya Super Eagles ya Nigeria.
Hii
inafwatia kauli ya chipukizi huyo ya kuasi timu ya taifa ya Uingereza
na badala yake kujiunga na vigogo wa soka ya Afrika Super Eagles ya
Nigeria.
Iwobi ameshajumuishwa katika kikosi cha Nigeria
kinachoratibiwa kuchuana dhidi ya Misri siku ya Ijumaa 26 -29 Machi
katika mechi ya kufuzu kwa kombe la mataifa ya Afrika.
England
imeanza harakati za kumshawishi asijiunge na Nigeria kwani hilo
litawanyima fursa ya kumshirikisha katika timu ya taifa ya England.
Iwobi
mwenye umri wa miaka 19 aliichezea England katika mashindano ya dunia
ya vijana wasiozidi umri wa miaka 16,17 na hata 18 kabla ya kuamua kuwa
angependa kuiwakilisha taifa alikozaliwa yaani Nigeria kuambatana na
kanuni za FIFA.
Jarida la Daily Mirror linaripoti kuwa harakati za
kimya kimya zinafanywa ilikumshawishi Iwobi abadilishe kauli yake kabla
ya Ijumaa, kwani akishaichezea Super Eagles itakuwa vigumu mno
kuichezea England katika mechi za kimataifa.
Iwobi amejumuishwa katika timu ya kwanza ya klabu yake ya Arsenal.