Kenya, Tanzania na
Sudan Kusini zitakuwa uwanjani hapo kesho kutafuta tiketi ya safari ya
Gabon mwakani kwa mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika..
Kenya
iko ugenini dhidi ya Guinea Bissau kundi E, Tanzania imesafiri Chad kwa
mechi ya kundi ya la G huku Sudan Kusini ikiikaribisha ikiikaribisha
Benin mechi ya kundi C..Mechi zingine zitakazochezwa kesho ni Sao Tome wako nyumbani dhidi ya Libya kundi F na Zambia wanakaribisha Congo kundi E, na kesho kutwa mechi ya kundi la B, Madagascar inapambana nyumbani na Afrika ya Kati..
Harambee Stars ya Kenya itakuwa na wachezaji wake wa kutegemewa wa ng'ambo wakiongozwa na kiungo mkabaji wa Southampton Victor Wanyama, kipa Arnold Origi na Michael Olunga.
Nahodha mpya wa Taifa Stars ya Tanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu ni tegemeo kubwa kwenye mechi yao na Chad.
Taifa Stars ni ya tatu kundi G na pointi moja tu kwa mechi mbili walizocheza, kwanza wakameza mabao matatu bila jibu kisha wakaenda sare na Super Eagles ya Nigeria.
Misri inaongoza kundi hilo na pointi sita, Nigeria ya pili na nne..
Sudan Kusini inashikilia nafasi ya pili kundi C na pointi tatu huku Mali ikiwa juu na nne, Benin ya tatu na Equatorial Guinea ya mwisho..
Mechi za marudiano zitachezwa wikendi hii kwa wanaocheza leo...
EmoticonEmoticon