Raymond Moore
Mkurugenzi mkuu wa
maandalizi ya michuano ya tenisi huko Indian Wells Raymond Moore
amejiuzulu baada ya matamshi yake yaliozua utata kuhusu wanawake katika
mchezo huo.
Moore mwenye umri wa miaka 69,amesema kuwa mchezo wa
tenisi wa wanawake unategemea sana wanaume,maoni yalioelezewa kuwa ya
ubaguzi wa jinsia na muungano wa tenisi nchini Marekani USTA.Mchezaji nambari moja duniani kwa upande wa wanawake Serena Williams alisema kuwa matamshi ya Moore yana kera na yasio ya ukweli.
Lakini mwenzake kwa upande wa wanaume Novak Djokovic alidai kuwa ziara yake inafaa kupigania wanaume wapewe fedha zaidi.
Lakini mchezaji huyo wa zamani wa Afrika Kusini baadaye aliomba msamaha kwa matamshi yake.
Gwiji wa mchezo huo Martina Navratilova alisema kwamba matamshi ya Moore yanachukiza sana,akiongezea kuwa wachezaji wanawake huenda wakasusia michuano ya Indian Wells iwapo Moore ataendelea kuwa mwandalizi.
Lakini raia huyo wa Serbia mwenye umri wa miaka 28 alihoji kwamba wanaume wanafaa kupewa fedha zaidi kwa sababu watu wengi huangalia mechi zao.
EmoticonEmoticon